Makala hii inaeleza jinsi ya kushusha na kufunga Firefox juu ya Mac..
- Ikiwa unaboresha kutoka toleo la awali la Firefox, angalia Kusasisha Firefox na toleo la karibuni.
Kufunga Firefox juu ya Mac
- Tembelea ukurasa wa kushusha Firefox katika kivinjari yoyote (kwa mfano, Apple Safari). Hiyo moja kwa moja itachunguza jukwaa na lugha kwenye kompyuta yako na kupendekeza toleo bora ya Firefox kwa ajili yako.
- Note: Kama unataka kuwa na uchaguzi wa lugha ya Firefox yako, tafadhali tembelea ukurasa wa kushusa mifumo na lugha.
- Bonyeza kifungo cha kijani kushusha Firefox.
- Mara shusha imekamilisha, faili ya (Firefox.dmg) inapaswa kufungua peke yake na hapo kufungua dirisha la Finder zenye programu za Firefox. Kokota ikoni ya Firefox juu ya folda ya Programu ili kuunakili huko.
- Kumbuka:Kama hauoni dirisha hii, bofya failiya Firefox.dmg iliyopakuliwa kuifungua.
- Baada ya kukokota Firefox kwa folda ya Programu, shikilia chini kitufe cha control huku ukibofya katika dirisha na kuchagua kutoka orodha.
- Unaweza kuongeza Firefox kizimbani mwako kwa urahisi. Fungua folda ya Programu yako na ukukote Firefox hadi kizimbani.
- Firefox ipo tayari kwa matumizi. Bonyeza tu juu ya picha yake kizimbani kuanzisha.
Kuanzia Firefox kwa mara ya kwanza
Wakati unpoanzisha Firefox kwa mara ya kwanza, utapewa onyo kwamba Firefox ilipakuliwa kutoka kwa mtandao. Kwa sababu wewe ulishusha Firefox kutoka tovuti rasmi, unaweza bonyeza
Pia, Firefox haitakuwa kivinjari cha msingi kwako na utaambiwa kuhusu jambo hilo. Hiyo ina maana kwamba wakati wa kufungua kiungo katika programu ya barua pepe yako, njia ya mkato ya mtandao, au hati ya HTML, 'haitafunguliwa' katika Firefox. Kama unataka Firefox kufanya mambo hayo, bonyeza kifungo